1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Vita vyapamba moto katika mkoa wa Donetsk

18 Septemba 2025

Vikosi vya Ukraine vinafanya mashambulizi ya kukabiliana na vikosi vya Urusi kwenye eneo la mashariki ambako Kiev inadai imeshayakombowa maeneo saba ya makaazi hadi sasa.

https://p.dw.com/p/50hig
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky asema wanajeshi wake wawafurushwa wanajeshi wa Urusi Donetsk
Picha: Julien Mattia/Le Pictorium/MAXPPP/picture alliance

Hivi leo Rais Zelensky ametembelea eneo la vita la Donetsk ambako vita vinaendelea kati ya vikosi vya Ukraine na Urusi.

Rais Zelensky hakutaja ni lini operesheni ya kijeshi ya Ukraine ilianzishwa huko Donestk lakini amesema  vikosi hivyo vimeshakombowa eneo la kilomita 160 za mraba tangu ilipoanzishwa na kwamba maeneo 9 ya makaazi yameshakombolewa na wavamizi kufurushwa na wanajeshi hao wa Ukraine.

"Kwa hakika wanajeshi wetu wanawanyima fursa wavamizi wetu kufanya operesheni ya mashambulizi makubwa ambayo wamekuwa wakiyapanga kwa muda mrefu na kuendelea nayo."

Watoa huduma ya matibabu wakiwa uwanja wa vita Donestk
Watoa huduma ya matibabu wakiwa uwanja wa vita Donestk Picha: Madeleine/ZUMA/IMAGO

Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha hali ilivyo kwenye uwanja wa vita  lakini Rais Zelensky akizungumza kwa njia ya Video amesema mapambano ni makali katika eneo la Dobropilia, ambako Urusi ilikuwa na udhibiti mkubwa kufikia katikati ya mwezi Agosti lakini pia kwenye eneo la Pokrovsk.

Donetsk ilishikiliwa kwa muda na Urusi

Mkoa wa Donetsk uliokaliwa kwa muda na Urusi lakini ambao Moscow inataka Kiev iuachilie kabisa kabla ya kufanyika mazungumzo yoyote ya amani, bado umebakia kuwa eneo linaloshuhudia mapigano makali.

Ukraine imesema droni zake zimeshambulia vituo vya kusafisha mafuta nchini Urusi katika kampeini yake ya mashambulizi yanayolenga kuvuruga sekta ya mafuta na gesi yaUrusi.

Hivi leo Urusi imeshambulia kwa bomu na kuuwa watu watano katika eneo linaloitwa Kostiantynivka kiasi kilomita 40 kutoka Dobropilia.

Ukraine imedai kushambulia vituo vya kusafisha mafuta vya Urusi
Ukraine imedai kushambulia vituo vya kusafisha mafuta vya UrusiPicha: ITAR-TASS/IMAGO

Urusi yajinadi kwenye luteka ya Zapad 

Wakati huo huo, wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi imesema inataraji kwamba maafisa wa kijeshi wa Marekani walioshiriki luteka za kijeshi hivi karibuni kwenye eneo la Zapad walifanikiwa kuona hali halisi inayoonesha kwamba Urusi sio kitisho kwa jumuiya ya kujihami ya NATO.

Luteka hiyo ya kijeshi ya siku tano iliyomalizika Jumanne wiki hii ilijumuisha mazoezi ya kijeshi yaliyohusisha silaha za kisasa za Urusi yakiwemo makombora ya masafa marefu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi  Sergei Lavrov
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei LavrovPicha: Sergei Bulkin/TASS/picture alliance

Wakati vita ikiripotiwa kupamba moto mashariki mwa Ukraine, kwengine waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, SergeiLavrov, amesema kwamba nchi hiyo iko tayari kufikia makubaliano juu ya mpango wa amani na Ukraine chini ya sharti kwamba maslahi ya Warusi ndani ya Ukraine yanalindwa.

Lavrov ameyasema hayo hivi leo kwenye mahojiano na shirika moja la habari la Urusi

 

Ruka sehemu inayofuata Video zetu fupi

Video zetu fupi